MAGARI YANAYOTUMIA UMEME RASMI 2040 HUKO CHINA.


Unaambiwa Katika mkakati wa kupunguza tatizo la Uchafuzi wa hewa yaani "Air Pollution".
China imesema ipo katika mkakati wa kupiga marufuku matumizi ya Magari yanayotumia Mafuta ya Petroli na Dizeli na Kutambulisha Magari Yanayotumia Umeme.

Naibu Waziri wa Viwanda Nchini humo alisema bado hawajaamua ni lini marufuku hiyo itaanza kutekelezwa.

"Hatua hizo bila shaka zitaleta mabadiliko makubwa katika sekta yetu ya Magari," alisema
Xin Guobin.

Kwa sasa Serikali ya China, Wanasayansi na Wataalamu wanafanya Utafiti wa kuwezesha suala hili ambalo linatarajiwa kuanza kutekelezwa ifikapo mwaka 2040 na teknolojia hii inatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa sana kwenye maendeleo ya Viwanda Duniani.

Nchi nyingine zenye mpango kama huu wa kuacha kutumia magari ya mafuta ni pamoja na Uingereza na Ufaransa.