SAMAKI MTU AONEKANA HUKO ISRAEL

Unaambiwa Watalii wengi wamekuwa wakimiminika kwenda huko Israel kumuona Nguva
(SAMAKIMTU)wakiamini labda na wao watamuona.
Na hii ni baada ya watalii waliokuwa pembezoni mwa Bahari hiyo kumuona nguva(SAMAKIMTU) akiwa juu ya mawe kutoka huko Kiryat Ya Israel.
Hata Hivyo ukweli ni kuwa Nguva  ni wanyama wakubwa wanaoishi baharini Na ni Mamalia wanaozaa Watoto walio hai na kuwalisha kwa maziwa. Nguva huwa na mikono ya mbele na mkia wenye umbo la pembetatu. Na hii huwafanya watu wengi kuamini kuwa ni Samakimtu.

Wanapatikana kwenye pwani za Bahari ya Hindi, Bahari ya Karibian, Afrika ya Magharibi na mto wa Amazoni na Wanaweza kufikia urefu wa mita 2.5 hadi 4 na uzito wa kg 1,500.