UNAAMBIWA HIKI NDIO KISIWA KIKUBWA ZAIDI KATIKA BAHARI YA PACIFIC NA KINAMILIKIWA NA MAREKANI

By, Maliquid Classic.

Kisiwa cha Guam ndio kikubwa zaidi katika bahari ya Pacific na kinamilikiwa na Marekani
Kisiwa hiki kina Mambo mengi sana Lakini haya ni mambo Sita ya Kushangaza kuhusu kisiwa hiki.
1. Ni eneo ambalo liko mbali zaidi kwa raia wa Marekani kutembelea bila kutoka Marekani.
Tumon Bay.


Image captLicha kumilikiwa na Marekani, kiko maili 8000 kutoka Marekani na inachukua takriban saa 19 kusafiri kwa ndege kutoka mji wa New York.

Wamarekani wanaweza kuelekea katika kisiwa hicho bila kutumia pasipoti.

2. Kila mtu aliyezaliwa kisiwani Guam ni Mmarekani lakini hawezi kumpigia kura Rais.

Tangu mwisho wa vita vya dunia , watu wawili waliokuwa wakiishi katika kisiwa hicho walipewa uraia lakini hawawezi kumpigia kura rais wa Marekani. Wana mwakilishi mmoja wa serikali laki yeye hana uwezo wowote kuhusu utengenezaji wa sera.
3. Guam ni kambi muhimu ya kijeshi.
Robo ya kisiwa hicho kinamilikiwa na jeshi la Marekani na kinatumiwa kama kambi ya Wanamaji na Wanaanga
Pia inakadiriwa kwamba karibia asilimia 10 ya Watu wa Guam wenye idadi ya 160,000 ni ya Wanajeshi.

4. Raia wa Guam wanajulikana kama Chamorro.

Chamorro ni jina la jumla lililopewa Watu wanaoishi katika Kisiwa cha Guam  na Watu wanaoishi katika Visiwa vya Micronesia katika Bahari ya Pacific.
Utamaduni wao unafanana na ule wa Uhispania zaidi ya Umarekani kwa sababu Uhispania ilidhibiti kisiwa hicho kwa takriban Miaka 300 hadi 1898.

5. Watu katika eneo hilo hawatozwi kodi.

Kuna sehemu Kubwa nne za Utalii.

Watalii kutoka Taiwan , Korea Kusini na Japan huchukua saa nne kusafiri hadi katika Kisiwa hicho kwa likizo ya kupata jua mbali na kununua vitu ambavyo havilipishwi kodi.

Maduka yote makubwa huuza bidhaa za mitindo na mengi hufunguliwa kwa saa 24 kwa siku.
6.  Ricardo Blas Jrndio mtu maarufu zaidi katika kisiwa cha Guam.
Mtu huyo mwenye Umri wa miaka 30 ni Mchezaji wa Judo ambaye alishiriki Judo katika Michezo ya Olimpiki ya 2008 na 2012 na alibeba Bendera ya Guam katika Mashindano yote lakini akashindwa kupata Medali licha ya kuwa mchezaji mwenye Uzani Mzito Zaidi wa Kilo 214.