BARUA YA WAZI KWAKO “MSANII CHIPUKIZI” JIFUNZE HAYA KUTOKA KWA BINTI “NANDERA”.



Yule Binti Wa “I’m Confident” Kabla Ya Kugusagusa Vionjo Wa Mziki Wakati Akitafakari Kuwa Na Ndoto Kubwa Alikutana Na Washikaji Wakamdanganya Kinouma. Akiwa Bado Anatafakari Wakavuruga Sana, Japo Mungu Akambariki Kwa Imani Kuu Ya One Day Kufikia Ndoto Zake.

.

Haswa, Yule Binti Wa Fundi Makenika Kutoka Kasikazini Mwa Tanzania Faustina Charles Mfinanga (NANDY) Hii Leo Anawakarisha #WatakaaTu Darasani Na Kutoa Somo Kubwa Kwa Wasanii Chipukizi.

.

Ndio, Uchache Wa Wasanii Wa Kike Tanzania Na Changamoto Wanazopitia Amezivunja Na Leo Anazidi Kuonesha Njia Kwa “Wasanii Chipukizi” Na “Wakongwe” Kwa Kukusanya Nyota Ili Kuutengeneza Mwezi.

.

Jicho Langu Limeona Mambo Mengi Ya Kujifunza Kutoka Kwa Binti Huyu Kwa Wasanii Haswa wanaochipukia Na Kwa Ufupi Chukueni Nondo Hizi..

.

1. Ubunifu: Toka Ameingia Rasmi Kwenye Uwanja Huu Ametengeneza Team Makini Na Yenye Ubunifu Wa Hali Ya juu. Team Ina Majukumu Na Uongozi Bora Kabsa.

.

2. Kujitoa: Binti Nandela Anajituma Si Mchezo, Anatoa Mashavu Kwa Waandishi Wa Nyimbo, Hana Roho Ya Korosho Na Hili Ni Somo Kubwa “Ukitaka Kubebwa Lazima Ujibebe Kwanza”.

.

3. Kujituma: Hapa Tazama Maandalizi Ya #WatakaaTu Mpaka Mwisho, Endelea Kuangalia Hadi Pale Mwanga Kigoma. Utajifunza Mwenyewe.

.

4. Nidhamu: Huu Ndo Msingi Wa Mafanikio Ya Binti Huyu, Amepitia Changamoto Nyingi Na Kubwa. Ameendelea Kuwa Na Nidhamu Na Muziki Wake.

.

5. Heshima: Mtazame Anavyozungumza na Waandishi Wa Habari,Anavyowazungumzia Wasanii Wakongwe Bila Shaka Utajionea Heshima Yake.

.

6. Kukubali: Anakubali Changamoto Na Kuzigeuza Kuwa Fursa. Rudi Kwenye Maandalizi Ya Hitsong Kubwa Kwangu #Leoleo. Habari Juu Ya Vile Vyombo Na Namna Alivyolipokea Lile Swala. Utajifunza Kitu

.

7. Muendelezo: Tangia Aanze Muziki Hajawahi Kukata Tamaa, Anatoa Hitsong Kuanzia Za Kidunia Mpaka Za Dini. Akiona Tobo Lolote Anaingia.

.

8. Kusikiliza: Mtazame Katika Interview Anazofanya, Press Conference. Yupo Makini Sana Na Ujibuji Wa Maswali,Yupo Kitaalamu Sana.

.

9&10. Kujiamini Na Kukaa Kimya: Si Kila Jambo Ni la Kujibu Na Kuongea. Busara Ni Muhimu. Wasanii JIFUNZENI.

@cloudsfmtz @officialnandy