“Sijawahi Tosheka Na Nilicho Nacho, Siku Zote Napambana Kupata Cha Juu Zaidi..Hii Kwangu Ndio Tafsiri Halisi Ya FURAHA”- Ni maneno ya nguli wa vipaji, mfanyabiashara na mkurugenzi wa British Entertainment Company synco, Bw.Simon Cowell.
.
Ukipata Pesa Kidogo Unatamani Nyingine, Ukisoma Unatamani Kusoma Tena, Unapata Mshahara Ukikosa Semina Unaroga, Ukinunua Vitz Unatamani Noah.. Hayo Ndo Maisha, Hakuna Anayetosheka Na Alicho Nacho..
.
Wakati Nakua Nilipenda Kusikiliza Muziki. Mama Yangu Alininunulia Redio Ya Casette, Ilikuwa Inadunda Hasa, Ni Juzi Tu. Midundo Mingi Ilikuwa Ni Kutoka huko India, Nilipenda Namna Walivyojipambanua Kwa Uwezo Wao Mzuri Wa Kuvuta Sauti “ Sauti Kinanda Na Mbilimbi”.
.
Ulipotoka wimbo wa "Uko Wapi" wa Nguli Na Fundi Rehema Chalamila aka Ray C, Niliacha Kusikiliza Midundo Ile, Midundo Ya Huyu Dada Ilikuwa Balaa, Sauti Usiombe, Uchezaji na mtindo wake wa KiunoBilaMfupa Nick Name Akapewa..
.
Alitusafirisha Kutoka Bara La Asia Mpaka Bara la Afrika, Huku Mashariki Tanzania , Kwa Utunzi Na Uimbaji Wa Kipekee. Alielimisha, Aliburudisha..Wengi Wanasifu Vipaji Vipya Kwenye Game Ya Music, Wanabeza Wasanii Wakongwe.. Hebu Niambieni Ni Nani Mwenye Uwezo Mkubwa Wa Kunisafirisha Kutoka India Mpaka Tanzania Kupitia Utunzi Na Sauti Yake Ya Mvuto Kama @rayctanzania Bila Shaka Kwa Kizazi Hichi Bado.
.
Bado Heshima Anayopewa RayC Haijaniridhisha.. Anaheshima Ya Kipekee Sana Kwenye Muziki Huu Wa BongoFlevaHisia..Apewe Heshima Yake..
.
Mpambanaji Mwenzangu Huku Kitaa, Uko Wapi, Mtaa Unakuita, Familia Inakuita, Watoto Nyumbani Wanakuita.. Wanangu Pambana, Tengeneza INDENTITY YAKO Hapo Kitaa Kama Ni Mkulima, Tengeneza Identity, Mfanyabiashara, Usitosheke’ Tengeneza Identity. Acha Alama Ya Upekee Kama RayC..
.
Kumbuka Hata Kama Wote Mnauza Nyanya Pale Tandika Sokoni , Yule Anayetengeneza Identity Ya Usafi, Nyongeza Na Lugha Ya Upekee Kwa Wateja Huwa Anashinda Sana Wateja..