Kijana mmoja kutokea Myanmar Burma amevunja Rekodi ya Dunia ya kuwa kijana wa kwanza kuripotiwa na vyombo vya habari kuwabeba Wazazi wake Baba na Mama kwa Siku Saba.
Wazazi hao ambao ni Wazee sana walibebwa na mtoto wao Kutoka Myanmar Burma kwenda Bangladesh ili kuwaokoa na mauaji ya kikatili yanayofanywa na Wanamgambo dhidi ya Waislamu na safari hiyo imechukua takribani siku Saba Kuimaliza.
Kijana Huyo aliwabeba wazazi wake kwenye matenga mawili aliyoyafunga kwenye mti mmoja na kuupitisha mti huo begani.