NYUKI WAVAMIA MKUTANO WA JUBILEE


Unaambiwa, Kulingana na gazeti la The Standard, Nyuki walitibua mkutano wa kisiasa wa chama Tawala cha Jubilee nchini Kenya katika kaunti ya Taita-Taveta yapata kilomita 360 kutoka mji mkuu wa Nairobi.

Wafuasi wa chama hicho walilazimika kukimbilia usalama wao wakati nyuki hao walipowavamia , Hatahivyo nyuki hao walipotea baada ya maombi kufanywa na mwanasiasa mmoja.

Wanasiasa walilaumu shetani kwa uvamizi huo wa mkutano huo uliofanyika katika mji wa Wundanyi ,ulioitishwa kumuunga mkono rais Uhuru Kenyatta kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26.

Mahakama ya juu nchini humo ilifutilia mbali ushindi wa rais Uhuru Kenyatta dhidi ya kiongozi wa upinzani Raila Odinga mnamo tarehe 8 mwezi Agosti ikisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa na makosa chungu nzima ikiwemo udanganyifu.

Ikumbukwe Nyuki wengine waliwavamia maafisa wa polisi na watu wengine nje ya mahakama katika mji mkuu wa Nairobi , wakati majaji walipotoa uamuzi wao kamili kuhusu kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi huo tarehe 20 mwezi Agosti.