MIGOGORO YA NCHI NI KIKWAZO KATIKA MASOMO YA WANAFUNZI HASA WASICHANA.

Unaambiwa, Takwimu kutoka Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa wasichana wanauwezekano mara mbili zaidi wa kukosa masomo katika maeneo yenye mizozo.

Katika nchi zilizo na migogoro, familia nyingi zinakumbwa na hali ya umasikini, afya duni, lishe duni na kukimbizwa makwao kutokana na vita na mizozo, Hivyo Wasichana wengi wadogo hufanya kazi badala ya kwenda shuleni na wengi huolewa wakiwa wachanga na kuzima fursa yoyote ya kupata masomo.
 Takwimu hizo zilijikita katika kuangalia; Idadi ya wasichana wasiokuwa na nafasi katika shule za msingi, Idadi ya wasichana wasiokuwa na nafasi katika shule za sekondari, Idadi ya wasichana wanaohitimu kutoka shule za msingi, Idadi ya wasichana wanaohitimu kutoka shule za sekondari, Miaka ambayo wasichana huanza kwenda shule, Idadi ya wanawake wasiojua kusoma na kuandika, na Idadi ya walimu ikilinganishwa na wanafunzi.

Hizi hapa sehemu 10 ambazo wasichana hupata changamoto za kusoma:
  •     Sudan kusini: Zaidi ya robo tatu ya wasichana hawakufika shule ya msingi.
  •     Jamhuri ya Afrika ya Kati: kuna mwalimu mmoja kwa wanafunzi 80
  •     Niger: Asilimia 17 pekee ya wanawake kati ya miaka 15 na 24 wanaweza kusoma na kuandika
  •     Afghanistan: Kuna pengo kubwa la jinsia huku uwezekano wa wavulana kuwa shuleni kuliko wasichana ukiwa juu
  •     Chad: Masuala ya kijamii na uchumi inawazuia wasichana na wanawake kupata masomo
  •     Mali: Asilimia 38 pekee ya wasichana huweza kuhitimu kutoka shule za msingi.
  •     Guinea: Wastani wanaotumia wanawake zaidi ya miaka 25 katika masomo ni chini ya mwaka mmoja
  •     Burkina Faso: Asilimia 1 pekee ya wasichana humaliza masomo ya sekondari
  •     Liberia: Takriban theluthi mbili ya wanafunzi waliotimia umri wa kuenda shule za msingi hawaendi shuleni
  •     Ethiopia: Wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikia umri wa miaka 18
Hatahivyo, Ukosefu wa walimu wa kutosha ni tatizo ambalo lilishuhudiwa kwenye nchi masikini.
Ikumbukwe Mwaka jana, Umoja wa Mataifa ulisema kuwa walimu milioni 69 zaidi, wanastahili kuajiriwa Duniani kufikia mwaka wa 2030 ikiwa ahadi za kimataifa kuhusu masomo zitahitajika kutimizwa.