WATOTO MILIONI 124 DUNIANI NI WANENE ZAIDI.

Unaambiwa, kwa mujibu wa utafiti mpya idadi ya watoto na vijana walio na uzito mkubwa wa mwili imeongezeka mara dufu, ikimaanisha kuwa watoto milioni 124 kote duniani ni wanene zaidi.

Kulingana na jarida la Lancest idadi hiyo ndiyo kuwa zaidi ya aina yake na inaangazia visa vya unene wa mwili kwa zaidi ya nchi 200.

Nchini Uingereza moja kati ya vijana 10 walio kati ya umri wa miaka 5 na 19 wako na unene mkubwa wa mwili, Watoto walio na unene mkubwa wa mwili wana uwezekano wa kuendelea na hali hiyo wanapokuwa watu wazima na kuwaweka katika hatari kubwa ya kiafya kwa mujibu wa wataalamu.

Hii ni pamoja na aina mbili za ugonjwa wa kisukari, ugonjwa wa moyo, kiharusi na aina fulani ya saratani kama vile ya matiti .
Licha ya viwango vya unene wa juu wa mwili kuonekana kudhibitiwa kwenye nchi nyingi zenye kipato cha juu barani Ulaya ikiwemo Uingereza, viwango hivyo vinazidi kuongezeka katika nchi zengine dunia, kwa mujibu wa watafiti hao.

Hatahivyo, Watafiti wanaamini kuwa kuwepo kwa vyakula vya bei ya chini vya kenenepesha ni moja ya sababu na Idadi kubwa ya watoto na vijana walio na unene wa juu wa mwili imeshuhudiwa mashariki mwa Asia, China na India zimeshuhudia viwango hivyo vikiongezeka miaka ya hivi karibuni.

Watafiti wanasema kuwa ikiwa hali iliyo sasa duniani itaendelea ,basi watu walio na unene wa juu wa mwili watawazidi wale walio na unene wa chini. Idadi ya wasichana na wavulana walio na uzito wa chini wa mwili imekuwa ikipungua tangu mwaka 2000.