Unaambiwa, Kichwa cha mwandishi wa Sweden Kim Wall aliyotoweka miezi miwili kimepatikana baharini huko Sweden.
Mara ya wisho Bi Wall, 30, alionekana akiwa hai jioni ya Agosti 10 wakati alipokuwa akiondoka na bwana Marsden katika manowari.
Waogeleaji walipata mifuko iliokuwa na kichwa chake, miguu na nguo katika eneo la Koge Bay kusini mwa mji wa Copennhagen kulingana na inspekta mkuu wa polisi wa eneo hilo Jens Moller Jensen.
Aidha Matokeo ya uchunguzi yamebaini kwamba kichwa hicho ni cha Bi Wall na kwamba hakina ishara za kwamba fuvu lake la kichwa liliumizwa ama kupigwa.
Matokeo hayo yanaenda kinyume na taarifa za Marseden kwamba alifariki baada ya kugonga kichwa chake katika mlango.
Awali bwana Marsden alisema kuwa alimsafirisha na kumwacha akiwa salama mjini Copenhagen , lakini baadaye akabadilisha taarifa yake na kusema kwamba alimzika baharini baada ya ajali mbaya.
Hatahivyo Bwana Marsden mwenye umri wa miaka 46 amekana kumuua huku akisema mabegi hayo yaliopatikana yalikuwa yamechanganywa na kupimwa uzani na vipande vya vyuma.