HUYU NDIYE MNYAMA ANAYELALA KWA MUDA MFUPI ZAIDI DUNIANI

UnaambiwaNdovu Ndiye Mnyama Anayelala Kwa Muda Mfupi Zaidi Duniani.
Utafiti Uliofanywa na Wanasayansi kutoka nchini Botswana waliowafuatilia Ndovu wawili wamebaini kuwa  wanyama hao hulala muda mfupi  zaidi ya mnyama mwingine yeyote duniani.

Ndovu hulala kwa saa mbili pekee hususani nyakati za usiku na Wakiwa katika hifadhi hulala kati ya masaa nne hadi sita kwa siku.
Ndovu wakiwa viongozi wa familia zao mara nyingine husalia macho kwa siku kadhaa na huonekana wakifunga macho ama kuota mara moja kila siku tatu ama hata nne.

Hata hivyo sifa pekee ya Wanyama hao ni kuwa na uwezo mkubwa wa kukumbuka vitu vilivyopita japo haijulikani kwa nini wanyama hao wanaweza kuishi kwa kulala kwa muda mfupi licha ya usingizi kuwa na umuhimu mkubwa katika ubongo.