MWANAUME MMOJA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMGUSA KIUNO MWANAUME MWENZAKE


Unaambiwa, Jamie Harron, ambaye ni raia wa  Scotland kutoka Stirling alifikishwa mahakani leo Jumapili baada ya kuripotiwa kukosa kufika mahakamani awali kwenye mji huo.

Mwanamume huyo anakabiliwa na kifungo cha miaka 3 mjini Dubai baada ya kugusa kiuno cha mwanamume mwingine ndani ya baa.

Jamie Harron mwenye umri wa miaka 27, alikamatwa kwa kuonyeha tabia mbaya hadharani, kufuatia kisa kwenye baa ya Rock Bottom mjini Dubai tarehe 15 mwezi Julai.

Harron ambaye alikuwa akifaya kazi huko Afghanistan, alisimama mjini Dubai kwa siku mbili wakati kisa hicho kilitokea.

Anasena alikuwa anajaribu kuzuia kumwaga kinywaji chake kwenye baa iliyokuwa imejaa watu, kwa kuweka mikono mbele wakati alipomgusa mwanamume mmoja kimakosa kwenye kiuno katika harakati za kuepuka kumgonga.

Anaripotiwa kuzuiwa siku tano katika gereza la Al Barsha kabla ya kuachiliwa kwa dhamana ambapo pia alinyanganywa passpoti yake.