PUNGUZA VIFO VYA GHAFLA KWA KUMLAZA MTOTO CHALI.

 
Unaambiwa, Kufuatia taarifa Iliyoripotiwa na CNN siku za karibuni akina mama wameshauriwa kuzingatia namna ya kuwalaza watoto ili kupunguza vifo vya ghafla.

Wanawake Wengi wamezoea kuwalaza watoto Kifudifudi na ili kupunguza hatari ya matatizo ya vifo vya ghafla vya watoto yaani Sudden Infant Death Syndrome ‘SIDS’ ni vyema wakawalaza Chali.

Inashauriwa kuwa watoto walio na umri wa chini ya mwaka mmoja ni vizuri wakalazwa chali kwani wako kwenye hatari ya kukosa hewa vizuri au kupaliwa pindi wanapokua wamelazwa kifudifudi na wakapoteza maisha

Imeripotiwa kuwa kwa mwaka 2015 zaidi ya watoto 1600 nchini Marekani walikufa vifo vya ghafla kwasababu ya kulazwa kwa namna hiyo.