MAMBO HAYA YANAWEZA KUKUTIA NGUVUNI DUBAI.

Unaambiwa,  Shirika linalofahamika kama Detained in Dubai linawaonya wageni wanaouzulu mji huo kwamba wanaweza kutiwa nguvuni kwa tabia zifuatazo ambazo huenda ni za kawaida nchini mwao kama vile:
  • Kutembea hadharani ukiwa umeshikana mkono ama kumbusu mtu kwenye shavu hadharani.
  • Kulala chumba kimoja na mtu ambaye ni wa jinsia tofauti ambaye hamjaoana
  • Kushiriki ngono na mtu wa jinsia sawa na yako
  • Kubishana ama kuonyesha dharau kwa mtu mwingine
  • Kuapa ama kuonyesha ishara za ukatili
  • Unywaji wa pombe hata katika maeneo yaliyoidhinishwa
  • Kuvaa mavazi ya kubana mwili kama vile suruari za jinzi
  • Kwa mwanamke kutofunika mikono ama miguu yako
Jiji la Dubai linasifika sana kwa vivutio vingi vinavyowafanya watu wengi Duniani kwenda kutembea, kufanya shopping wengine wanaenda kwa ajili ya mapumziko tu.