HESHIMA ALIYOPEWA RAIS JACOB ZUMA YAKOSOLEWA.


Unaambiwa, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amepewa heshima kubwa Wakati wa ziara katika jimbo lililopo kusini mashariki la Imo nchini Nigeria siku ya Jumamosi na Jumapili kwa kupewa cheo cha kiongozi wa kitamaduni ambacho ndicho cha juu zaidi kinachotolewa eneo hilo, Pamoja na kujengewa sanamu kubwa ya shaba na kuipa barabara moja jina lake. .

Kutokana na kupewa Heshima hiyo, Muungano wa mashirika ya kupambana na ufisadi (CSNC) ambao ni wa zaidi ya mashirika 150 ya kupambana na ufisadi nchini Nigeria, umemlaani gavana wa jimbo hilo Rochas Okorocha, kwa kumtambua Zuma kama mtu shujaa mbele ya kundi la vijana wa Afrika, wakati anakabiliwa na shutuma nyingi za ufisadi nchini mwake.

Muungano Huo Uliandika Katika Taarifa kuwa "Ni kama Gavana Okorocha hafahamu kuwa watu wa Afrika Kusini kwa sasa, wanamtaka Rais wao ajiuzulu kwa kuleta aibu kwenye nchi ya Nelson Mandela?".