HII NDIO HISTORIA YA CHALE "TATTOO".


Chale Maarufu kama 'tattoo'huchanjwa au kuchorwa na watu wengi sana Duniani. Mara nyingi mchakato mzima huhusisha kuchomwa kwa sehemu ya juu ya ngozi na kujaza rangi kwenye chale.
Vijana wengi huchanjwa chale kuonyesha utambulisho wao, jambo ambalo linawatambulisha kwa njia ya kipekee hasa sifa zao halisi.

Chale au 'tattoo' hazijaanza kuchorwa miaka ya hivi karibuni, Unaambiwa;
   - Binadamu wamekuwa wakichanjwa chale kwa maelfu ya miaka.
   -Chale Zilitumiwa kuwatambua wafungwa, watumishi, vijakazi na watumwa.
   - Wagiriki na Warumi enzi za kale walikuwa na chale, India pia.
    -Wayahudi walichorwa chale zenye nambari za utambulisho walipokuwa wanazuiliwa na   kufanyikwa kazi na Wanazi waliokuwa wanatawala Ujerumani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
   -Chale Zilitumiwa pia kuwatambua binadamu na watu wa tabaka mbalimbali
   - Mara nyingi chale zilikuwa kama adhabu, na zilichukuliwa kama jambo la aibu au ishara ya kudunishwa.
    -Wakati mwingine, zilikuwa ishara ya kumilikiwa na mtu fulani - mfano chale yenye nembo au alama ya baba wa mtu au mume wa mtu.
     -Vifaa alivyotumia vilikuwa ni sindano na moto.

Unaambiwa,  kipindi hicho, hakukuwa na dawa za kupunguza maumivu au mafuta ya kuharakisha shughuli ya kupona na hivyo Chale wakati huo zilichukua mwezi mzima kupona.

Katika jamii nyingi maeneo ya mashambani katika jimbo la Uttar Pradesh kaskazini mwa India, ni lazima kwa wanawake ambao wameolewa kuwa na chale, ambazo kwa lugha yao hufahamika kama Godna.

Keya Pandey,huyu ni mwanaathropojia wa kijamii kwa sasa katika chuo kikuu cha Lucknow ambaye amefanya utafiti sana kuhusu chale katika maeneo ya mashambani India anasema michoro mingi huwa na maua na majani ya mimea mbalimbali.

Aidha alibainisha kuwa wengine huchanjwa chale za majina ya waume zao au baba zao na wengine huchorwa majina ya vijiji vyao au nembo za ukoo au ishara nyingine za kitamaduni, bila kusahau pia miungu.
Bi Pandey anasema ameona chale katika karibu kila jamii India na anakadiria kwamba mamilioni ya wanawake wana chale.