UNAAMBIWA WANAWAKE HUPOTEZA HAMU YA NGONO ZAIDI YA WANAUME

Utafiti uliofanywa Nchini Uingereza umeonesha kuwa Wanawake wana uwezo mkubwa wa kupoteza hamu ya kufanya Tendo la Ndoa.
Matokeo hayo yanatokana na mahojiano ya wanaume 5000 na wanawake 6,700 yaliochapishwa na shirika la BMJ Open.
Aidha Utafiti huo umebaini kuwa Wanaume hupoteza hamu ya tendo la ngono kutokana na umri wao Huku Wanawake wengi hupoteza hamu hiyo wanapoishi na wapenzi wao kwa muda mrefu.
Pia hali mbaya ya kiafya ni moja ya viathiri vikubwa vya kupoteza hamu ya Ngono.
Watafiti hao wamesema kuwa matatizo ya hamu ya ngono yanafaa kutibiwa kwa kumchunguza mtu badala ya kutumia dawa.

Kwa jumla asilimia 15 ya wanaume na asilimia 34 ya wanawake waliofanyiwa utafiti huo walisema kuwa walipoteza hamu ya tendo la ngono kwa muda wa miezi mitatu ama hata zaidi katika mwaka uliopita.
Kwa wanaume, ukosefu huo wa hamu ya ngono ulikuwa juu miongoni mwa wanaume wa kati ya umri wa miaka 35-44 huku kwa wanawake ukionekana kati ya umri wa miaka 55 na 64.