UNAAMBIWA HIVI NDIO VITU TISA VILIVYOVUMBULIWA NA WANAWAKE


1. Programu za Kompyuta - Grace Hopper
Baada ya kujiunga na jeshi la wanamaji la Marekani wakati wa Vita kuu vya Pili vya Dunia, Grace Hopper alipewa kazi ya kuunda kompyuta mpya, iliyopewa jina Mark 1.
Hakuchukua muda mrefu kabla yake kuwa miongoni mwa watengenezaji wa Programu za Kompyuta (maelezo ya kufanyiwa kazi na kompyuta) wakati wa miaka ya 1950.
Alishiriki katika kuunda compiler, programu ndogo ambayo iliweza kufasiri maelezo ya kompyuta ya kuandikwa na kuyafanya kuwa maandishi ambayo Kompyuta Ingeyasoma.

2. Kumtambua mpiga simu (Caller ID) na Kuichelewesha simu(Call waiting)- Dkt Shirley Ann Jackson
Image result for Dkt Shirley Ann Jackson
Dkt Shirley Ann Jackson ni mwanafizikia ya nadharia Mmarekani, ambaye utafiti wake miaka ya 1970 ulichangia kuanzishwa kwa huduma mbili, moja ya kumtambua anayepiga simu na nyingine ya kuichelewesha simu.

3. Mashine ya kuosha vyombo - Josephine Cochrane
Image result for Josephine Cochrane
Mtumbuizaji Cochrane alitaka mashine ambayo ingeosha vyombo vyake haraka kuliko wafanyakazi wake wa nyumba, na bila kuvivunja.
Mashine yake ilijumuisha mota iliyokuwa inazungusha gurudumu ndani ya mtungi wa kuchemsha maji ulioundwa kwa madini ya Shaba Nyekundu.
Ilikuwa ndiyo mashine ya kwanza kabisa ya kuosha vyombo iliyotumia presha ya Maji.

4. Kipangusa kioo cha gari - Mary Anderson
Image result for Mary Anderson
Siku moja majira ya baridi mwaka 1903, Mary Anderson alikuwa ziarani New York alipogundua kwamba dereva wake Wa gari lililokuwa limembeba alilazimika kila wakati kufungua kioo cha upande wake ili kupangusa theluji kwenye kioo cha mbele cha gari.
Kila wakati alipofungua kioo, hewa baridi iliingia ndani ya gari.
Anderson alianza kufikiria suluhu - bada lenye Mpira ambalo lingesongeshwa mtu akiwa ndani ya gari, na mwaka 1903 alisajili uvumbuzi wake.

5. Betri za kutumiwa anga za juu - Olga D Gonzalez-Sanabria
Image result for Olga D Gonzalez-Sanabria
Olga D Gonzalez-Sanabria, ambaye asili yake ni Puerto Rico, alisaidia kuasisi teknolojia ambayo ilisaidia kuundwa kwa betri hizo miaka ya 1980.
Betri zinazodumu na chaji muda mrefu za Nickel-hydrogen zimesaidia sana kutoa nishati kwa Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu.

6. Mfumo wa usalama nyumbani - Marie Van Brittan Brown
Marie Van Brittan Brown
Marie Van Brittan Brown, mwuguzi ambaye mara nyingi alikuwa akikaa pekee nyumbani, alifikiria kuhusu kituo ambacho kingemfanya kujihisi salama zaidi nyumbani.
Akiwa pamoja na mumewe Albert, Van Brittan Brown aliunda mfumo wa kwanza wa kuhakikisha usalama nyumbani kutokana na ongezeko la visa vya uhalifu na desturi ya polisi kuchelewa kufika eneo la uhalifu miaka ya 1960.
Kifaa chake kilikuwa na vitu vingi, kilikuwa na kamera ambayo ilitiwa nishati na mota. Kamera hiyo ilipanda na kushuka na kutazama nje kupitia tundu la kuchungulia.
Kulikuwa na skrini kwenye chumba chake cha kulala ambacho kilikuwa pia na kitufe cha kufungulia king'ora.

7. Kutenganisha seli tete - Ann Tsukamoto
Image result for ann tsukamoto
Uvumbuzi wake ulisajiliwa rasmi 1991 na tangu wakati huo, kazi yake Tsukamoto imesababisha kupigwa hatua kubwa sana katika kufahamu mfumo wa damu wa wagonjwa wa Saratani, jambo ambalo mwishowe huenda likasaidia kugunduliwa kwa Tiba.

8. Kevlar - Stephanie Kwolek
Image result for kevlar - stephanie kwolek
Mwanakemia huyu alivumbua nyuzi zisizo na uzito sana ambazo hutumiwa katika fulana zinazozuia risasi kupenya pamoja na mavazi mengine ya kukinga mwili dhidi ya Risasi.
Tangu uvumbuzi wake mwaka 1965, nyuzi hizo ambazo zina nguvu mara tano kuliko chuma, zimesaidia kuokoa maisha ya watu wengi.

9. Monopoly - Elizabeth Magie
Image result for elizabeth magie
Mwanaume kwa jina Charles Darrow hutambuliwa kama mwasisi wa mchezo maarufu zaidi wa ubao duniani, lakini kanuni zake zilivumbuliwa na Elizabeth Magie.
Magie alitaka kuonyesha matatizo ya ubepari kwa mchezo mpya ambapo wachezaji wakebadilisha pesa na mali bandia.
Muundo wake ambao aliusajili mwaka 1904 uliitwaThe Landlord's Game.