HIZI HAPA BARUA ZA BARACK OBAMA KWA MPENZI WAKE WA ZAMANI

Unaambiwa, Barua zilizoandikwa kwa Mkono kati ya Barack Obama alipokuwa mdogo na mpenzi wa wakati huo Alexandra McNear ambaye alikutana naye katika jimbo la California, Zimechapishwa kwa mara ya kwanza tangu zichukuliwe na  Maabara ya chuo kikuu cha Emory University mwaka 2014.

Mkurugenzi wa maabara hiyo Rosemary Magee alisema, Barua hizo ziliandikwa vizuri na zinafichua utambulishi wa kijana huyo, Pia baadhi ya Barua hizo zinaonyesha hali ngumu ya maisha na kazi aliyofanya ambayo hakuipenda.

Barua hizo ziliandikwa kati ya 1982 na 1984 miaka mitano kabla ya Obama kukutana na mkewe Michelle Obama.
Katika mojawapo ya Barua hizo aliandika: "Naamini unajua kwamba natamani kukuona na kwamba wasiwasi wangu kwako ni mkubwa kama vile hewa, Matumaini yangu kwako ni sawa na kina cha bahari, penzi langu ni kubwa kwako". Ilitiwa saini: Mpenzi Barack.

Kufikia 1983, alimwambia: Nakufikiria kila mara ijapokuwa nakanganyika kuhusu hisia zangu. Inaonekana tutataka kuwa na kile ambacho hatutakipata , na hicho ndio kinachotuunganisha na ndicho kinachotutenganisha.

Katika barua moja, Obama aliandika kuhusu marafiki zake waliokuwa wanajiandaa kuanza maisha ama kusimamia Biashara za Familia zao.