MWIZI AIPONGEZA POLISI KWA KUMKAMATA


Anaitwa Boubacar Diallo mkazi wa Guinea ambaye pia ni mwanafunzi katika Chuo cha ufundi cha Mamou na mwizi mwenzake wamekiri wenyewe kwamba waliiba kiasi cha franga milioni 50 pesa za Guinea ambazo ni sawa na dola 5,600 kutoka kwenye duka la simu eneo la kaskazini magharibi mwa mji huo.

Diallo ameipongeza Polisi kwa kumpata na kusema kuwa polisi wapewe raslimali zaidi za kazi yao kwa kuwa ni wenye mafunzo mazuri si mchezo.

Aidha ameongeza kuwa hakuwahi hata siku moja kufikiria kwamba anaweza kukamatwa haraka na akasema anajuta kwa uhalifu wake na kuapa kutoiba tena.
Mpaka sasa  Boubacar Diallo anashikiliwa na polisi kutokana na wizi huo.