WALIODUMU KATIKA NDOA KWA MIAKA 75 WAFARIKI SIKU MOJA

George Spear mwanajeshi wa zamani Wa Uingereza na Jean Spear walikutana mwaka 1941 karibu na London wakati George akitoa huduma zake nchini Uingereza wakati wa vita Kuu ya pili ya Dunia.

Wanandoa hao walifunga pingu za maisha mnamo mwaka 1942 na hadi mwezi wa nane 2017 walitimiza miaka 75 ya ndoa yao Na mwezi mmoja tangu washerekee ndoa hiyo Wamefariki Siku moja wakiachana kwa Saa tano tu.

Wawili hao walifariki kwenye hospitali ya Ottawa siku ya Ijumaa baada ya Bi Spear mwenye umri wa miaka 94 kulazwa katika hospitali ya Queensway Carleton siku ya Jumatano siku moja baada ya mke wake kulazwa na kulala usingizi mkubwa.

Wahudumu wa hospitali walijaribu kumhamisha Bw Spear kwenda chumba alichokuwa mkewe, lakini kabla ya hilo kufanyika Bi Spear akafariki siku ya Ijumaa mwendo wa 04:30. Bwana Spear naye alifariki muda mfupi baadaye mwendo wa saa 09:45 akiwa na umri wa miaka 95.
Wanandoa hao wameacha watoto wawili wakubwa ambao ni Heather na Ian.

Enzi za uhai wao, Bi Spear na mume wake walikutana na Duke na Duches wa Cambridge wakati walipoitembelea familia ya Kifalme mwaka 2011.