KUWA NA MTOTO KUNACHANGIA KUISHI MIAKA MINGI

Unaambiwa Wataalamu kutoka Taasisi ya Karoliska mjini Stockhom nchini Sweden walifuatilia
maisha ya mtu kutoka umri wa miaka 60
kwa Wanaume wote (704,481), na Wanawake (725,290) waliozaliwa kati ya mwaka 1911 na 1925 wanaoishi nchini Sweden.

Waligundua kuwa Wanaume na Wanawake ambao walikuwa na takribani mtoto mmoja walikumbwa na vifo vichache kuliko wanaume na wanawake wasio na watoto.
Katika umri wa miaka 60 tofauti ya miaka ya kuishi kati ya wale walio na watoto na wasio nao ni karibu miaka miwili kwa wanaume na mwaka mmoja nusu kwa wanawake. Ikifika miaka 60, wanaume walio na watoto hutarajia kuishi miaka mingine 20.2 huku wanaume wasio na watoto wakitarajia kuishi miaka 18.4 zaidi ambayo ni tofauti ya mwaka moja nusu.

Nao wanawake walio na umri wa miaka 60 walio na watoto hutarajia kuishi miaka 24.6 zaidi huku wale wasio na watoto wakitarajia kuishi miaka 23.1 zaidi ambayo ni tofauti ya mwaka moja nusu.
Hata hivyo wazazi walio na watoto huishi maisha ya afya zaidi kuliko wale wasio na watoto.

Utafiti wa awali ulionyesha kuwa watoto wasichana ndio wanaweza kuwasaidia wazazi wao uzeeni kuliko hata watoto wavulana. Nao utafiti mpya unaonyesha kuwa wavulana wanaweza kuwasaidia wazazi sawa na wasichana ikiwemo kuwasaidia kupata matibabu.