Unaambiwa, Dmitry Baksheev mweye umri wa miaka 35 na mke wake Natalia wa nchini Urusi, walikamatwa baada ya mwili uliokuwa umekatwa katwa kupatikana kwenye kambi ya jeshi ambapo wawili hao walikuwa wanaishi. Wanandoa hao walikamatwa kwenye mji ulio kusini magharibi mwa Urusi wa Krasnodar, wamekiri kuua hadi watu 30.
Polisi walithibitisha kuwa bidhaa kadhaa za chakula na nyama vilivyopatiakan nyumbani kwao vinachunguzwa ikiwa vina DNA ya binadamu. Aidha Picha moja iilyochapishwa na vyombo vya habari nchini Urusi ilmuonyesha Bw Baksheev akiwa na sehemu ya mwili wa binadamu kwenye mdomo wake Na simu yao ya mkononi ilipatwa na wajenzi wa barabara mapema mwezi huu ikiwa na picha za miili iliyokuwa imekatwa katwa.
Picha moja ni ya tarehe 28 Disemba mwaka 1999 na inaonyesha kichwa cha binadamu kikiwa kwenye sahani pamoja na tunda. Aidha Mwili wa mwanamke mwenye umri wa miaka 35 uliripotiwa kupatikana katika chuo cha kijeshi ambapo wawili hao wanapoishi na ulipatikana na mkoba wa muathiriwa.
Wizara ya mambo ya ndani nchini Urusi ilithibitisha kuwa mwanamume aliye kwenye picha hizo ametambuliwa na kukamatwa na pia polisi walionekana katika picha wakisaka nyumba ya wawili hao.
Vyombo vya habari vinasema kuwa picha zilizopatikana zimechapishwa kwenye ukuta na kwenye simu zilionyesha kuwa mauaji hayo huenda yalianza karibu miongo miwili iliyopita.