TEKSI NDEGE YAZINDULIWA


                    Hati miliki ya picture ni Reuters.
Unaambiwa, Moja Ya Nchi zenye malengo makubwa ya kuwa Nchi za kiteknolojia Duniani ni Dubai  na mpango mkubwa ukitajwa kuwa ni ndege zisizo na rubani na roboti.

Sasa, Dubai imefanya jaribio la teksi ndege  ya kwanza  isio na Rubani ambayo wanatumaini itatumika kama chombo cha uchukuzi mijini. Ndege hiyo ilitazamwa ikipaa angani na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed. Ndege hiyo isio na rubani ina nafasi ya watu wawili iliruka kwa dakika tano katika pwani ya Ghuba.

Ndege hiyo ya teksi ilibuniwa na kampuni ya Ujerumani ya Volocopter na kampuni hiyo imesema inatumai kwamba ndege hiyo itaanza kufanya kazi katika kipindi cha miaka mitano. Naye Afisa mtendaji wa kampuni hiyo Florian Reuter amesema utumizi wake utahusisha simu aina ya Smartphone, programu kwa kuiagiza ndege hiyo kuruka hadi unapotaka kwenda.

Awali Teksi ndege isiokuwa na rubani ilifanyiwa majaribio nchini Ujerumani mnamo mwezi Aprili. Kwa Upande Mwingine, Kampuni pinzani ya China eHand ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuzindua msafara wa teksi ndege mjini humo lakini mipango yake ikaonekana kuchelewa.

Mtaalam wa roboti katika chuo kikuu cha Sheffield Noel Sharkey alisema kuwa changamoto kuu ni kama vile kukwepa teksi nyengine, majumba marefu, vindege na ndege zisizokuwa na rubani ambazo zinatumika kusafirisha mizigo.

Dubai imejiweka kuwa mji wa kiteknolojia Duniani ikiwa na mipango ya Magari ya kujiendesha kusimamia robo ya safari zote kufikia 2030.