WANAOAMBUKIZWA UKIMWI WAONGEZEKA.


Unaambiwa, Idadi ya watu wazima wanaoambukizwa virusi vya HIV Inazidi kuongezeka Ulaya.

Watafiti kutoka kituo cha kukabiliana na magonjwa cha Ulaya waliangalia matokeo ya vipimo kutoka nchi 31 kati ya mwaka 2004 na 2015.

Utafiti huo unazitaja nchi 16 zikiwemo Uingereza na Ujerumani kuwa ndizo zenye ongezeko kubwa la visa vya watu walio na zaidi ya miaka 50 wanaoambukizwa ugonjwa wa HIV.

Utafiti huo ulichapishwa kwenye jarida la Lancet, Na Waligundua kuwa mwaka 2015 karibu kisa kimoja kati ya visa vipya sita vilikuwa miongoni mwa watu walio na zaidi ya miaka 50, ikilinganishwa na kisa kimoja kati ya visa 10 miaka kumi iliyopita.

Vijana bado ndio wengi wanaopata maambukizi mapya ya ugonjwa wa HIV huku zaidi ya watu 300,000 walio kati ya miaka 15 na 49 wakipatikana na ugonjuwa wa hiu kote ulaya katika kipindi cha miaka 12 ya utafiti huo ikilinganishwa watu 54,000 wazee.

Hata hivyo uchunguzi huo hakuangalia kuhusu ni kwa nini watu wazima wanambukizwa sana na ugonjwa huo. Lakini uligundua kuwa maambukizi ni kupitia mapenzi ya watu wa jinsia moja na kuwa wanaume zaidi wanaambukizwa ugonjwa huo kuliko wanawake.