ASHIKILIWA KWA KOSA LA KUUA KISA MAKALIO YA MWANAMKE


Ramadhani Habibu ambaye ni mkazi wa kijiji cha Vilabwa, wilaya ya Kisarawe anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Pwani kwa madai ya kumchoma kisu mwenzake chanzo kikiwa ni ubishani wa makalio ya mwanamke aliyepita.

UnaambiwaRamadhani anadaiwa kumuua Emmanuel Nassor (26) kwa kumchoma na kisu kifuani baada ya kutokea ubishi kati yao kuhusu ukubwa wa tako la msichana aliyewapita wakipiga soga kijiweni.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani (ACP)Jonathan Shanna Alisema “Kuna mdada alipita sasa marehemu na mtuhumiwa walikuwa na wenzao kijiweni wakaanza kuzozana kuwa yule Mdada ana Chura wengine wakasema la kawaida ”. Ubishi ulikuwa mkubwa ndipo Ramadhani kwa hasira,akakimbia nyumbani kuchukua kisu alichokitumia kumchoma mwenzake hadi kumuua.

Mtuhumiwa alikimbia ambapo siku ya sept 27 majira ya saa 2.30 asubuhi alikamatwa
Kamanda Jonathan Shanna alieleza kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa kosa la mauaji .