AKAMATWA DUBAI KWA KUPANDISHA JUU KIDOLE CHA KATI

Unaambiwa, Jamil Ahmed Mukadam raia wa Uingereza anakabiliwa na uwezekano wa kushtakiwa kwa "tabia ya uhalifu wa maadili" kutokana na kitendo cha kunyanyua juu kidole cha kati cha mkono wake akimuonyesha dereva mjini Dubai.

Alikamatwa tarehe 10 Septemba katika uwanja wa ndege aliporejea Dubai kwa mapumziko mara ya pili ijapokuwa tukio lilitokea mwezi Februari mwaka huu na amesema kuwa aliamua kufanya hivyo baada ya kukasirika pale dereva alipompita barabarani.

Mukadam anafanya kazi  katika kitengo cha Teknolojia ya mawasiliano ya serikali ya Uingereza, amesema kuwa hakufahamu kuwa alikuwa na kesi ya kujibu aliporejea Dubai.
Aidha amesema kuwa ana hofu ya kuishiwa pesa kabla ya kesi yake kuanza na Pasipoti yake inashikiliwa kwa ajili ya kusubiri kesi yake jijini Dubai.