Wahenga wanasema “Mtembea bure si sawa na mkaa bure” msemo huu wa wahenga naufananisha na harakati mbalimbali za wasanii wa bongo katika kuteka hisia za mashabiki mbalimbali kuanzia watoto mpaka wazee ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.
Mziki wa bongo maarufu
kama Bongo fleva haijafahamika rasmi mpaka leo nani ni muanzilishi wake japo
kuna watu mbalimbali ambao inasemekana ndio waanzilishi rasmi wa mziki huu kama
Mike Mhagama mnamo mwaka 1996 ambaye alikuwa akijaribu kutofautisha mziki wa
R&B na HIPHOP wa marekani katika
kipindi cha Dj show kilichokuwa maarufu kwa kipindi kile.
Leo sitajikita
katika historia ya bongo fleva bali nimetua nanga yangu katika harakati za wasanii
mbalimbali katika kuteka hisia za mashabiki kuanzia bongo mpaka mamtoni katika
tambo zote kama Hiphop, R&b mpaka Afro pop na mziki unaotamba kwa sasa
maarufu kama singeli.
Nyota mbalimbali za
wasanii zilianza kung`aa tangu zamani katika ramani ya mziki ndani na nje ya
mipaka ya Tanzania . Kuna makundi yaliyong`aa katika ulimwengu huu wa bongo fleva
kama Kwanza Unit 1993 kundi lililotamba sana na mmoja wa wananchama ni Professa
Jay, hata hivyo kuna makundi mengine mengi kama East cost team, TMK wanaume, TMK Family.
Lady Jay Dee
maarufu kama komandoo ni nyota ya kwanza
kung`aa kwa upande wa wasanii wakike, alitoa album kama Machozi 2000
na ameshashinda tuzo mbalimbali kama video bora ya msanii wa kike channel O 2005
na best collaboration video (makini) with titi kutoka Uganda, 2003 channel O
music video awards, video of the year( machozi) na tuzo mbalimbali za Kilimanjaro Music Awards na hivyo kuwa nyota ya kwanza kung`aa kwa upande wa anga za kimataifa hasa Africa.
Juma Kassim
Ally Hii ni nyota nyingine iliyoanza kung`aa katika anga za kimataifa. Ana majina mengi maarufu kama Sir Nature, kiroboto,
kibla, msitu wa vina mwenye album kama nini chanzo 2001 ugali 2003 ubinadamu
kazi 2005 zote history 2006 ameshashinda tuzo mbalimbali za kimataifa kama
tuzo za channnel O kama wimbo bora wa Afrika mashariki – Mugambo 2007 na tuzo za kutosha za Kilimanjaro Music Awards.
Ambwene Allen
Yessayah maarufu kama A.Y ni moja ya nyota iliyoanza kung`aa mapema zaidi katika soko la Hiphop biashara
na kufanikiwa kujitwalia tuzo ya Best video from Tanzania 2007, Kisima Music
awards na wimbo wake wa usijaribu 2008 pearl of Africa music awards best
Tanzanian male artist , channel O music video awards as Best East African
video na tuzo kibao za Kilimanjaro Music Awards.
Kwa leo hizi ni nyota kadhaa zilizoanza kung`aa katika anga za kimataifa na kujitwalia tuzo mbalimbali.
Makala hii maalumu ya NYOTA ING`AAYO itakujia kila wiki hapahapa MALIQUIDHITZ hasa ikikuangazia wasanii wakali kutoka Tanzania waliofanya na wanaofanya vizuri nje ya mipaka ya Tanzania.