AMKA KIJANA

Na, James Pius.

Upo kama ulivyo Kwasababu Ulikwishaamini Utakuwa hivyo Ulivyo Tangu Jana. Na vile utakavyo kuwa kesho, itakuwa ni Matokeo ya jinsi uaminivyo leo kuhusu hiyo kesho. Nina uhakika leo yako Ilitegemea jinsi ulivyoishi jana yako na kesho yako Itategemea utakavyoishi leo yako.

Kijana fanya kazi kama Mtumwa ili Kesho yako uishi kama mfalme. Mungu aliwaumba watu wote kama Binadamu na si kama Tajiri au Masikini. Hakuna aliyetoka tumboni mwa Mama yake akiwa na chochote mkononi. Hali ya kutafuta mafanikio ipo mikoni mwako.

Wengine wanalalamikia mazingira waliyolelewa na kuzaliwa, swali ni je mazingira uliyolelewa au kuzaliwa ndio yanayosababisha ugumu ulionao, La hasha!!! Mazingira ya kuzaliwa au kulelewa yanaweza kutofautiana lakini suala la msingi ni, 
Je ni kiasi gani umedhamilia kupata mafanikio? na Je ni kiasi gani upo tayari kutumia fursa yoyote inayojitokeza mbele yako katika kutafuta mafanikio?.

JIFUNZE, Kuna watu maarufu walioheshimika na wanaoheshimika sana duniani ambao walitokea katika hali ngumu na familia duni. Chachu ya mafanikio yao wote ni kwamba waliamua na kudhamiria kutoka hatua moja hadi nyingine.

Nani asiyemjua Msanii maarufu wa Regge wa miaka hiyo ..LUCKY DUBE Msanii aliyejitwaalia umaarufu kupitia nyimbo mbalimbali za  harakati, mapinduzi na mapenzi, msanii ambaye Mama yake SARA alimpa jina la LUCKY kwa sababu alichukulia kuzaliwa kwake kama bahati baada ya mimba nyingi kutoka.

Haswa, Mwanamziki huyu alipitia shida nyingi kabla ya Mafanikio yake, alilima sana kama kibarua japo hakulipwa vizuri, ndipo alipoingia rasmi shuleni ( Umuhimu wa elimu) na akiwa shule alianza kuimba katika kwaya moja katika kikundi cha Sky Band na hapo alikuwa chini ya miaka 18 na alipofikisha miaka kumi na nane alijiunga na bendi ya Binamu yake, The love brothers. Harakati zake hazikuishia hapo LUCKY DUBE  pia alishafanya kazi kama Mlinzi katika Kampuni ya Hole na Cooke kama Mlinzi kwenye mnada wa Magari huko Midrand. FUNZO,  Chachu ya mafanikio yake ni kwamba aliamua na kudhamiria kutoka hatua moja hadi nyingine.

Mtaani kuna tatizo kubwa la Vijana wengi Wasomi kukaa na kusubiri kuajiriliwa na kushindwa kutumia maarifa waliyoyopata kwenye elimu yao katika mazingira yao. Kuna fursa ya Kilimo, Viwanda vidogo vidogo, Ubunifuu katika Biashara ambavyo ni chachu ya Mafanikio.

Mtaji umekuwa kimbilio la utetezi kwa Vijana wengi, lakini hao hao husahau kabisa juu ya kuendeleza maarifa waliyonayo.
JADAV PAYENG, Baada ya kurudi kijijini kwao kulikokuwa na ukame uliokithiri huko katika kisiwa cha MAJULI, INDIA alianza ratiba ya kupanda Mti mmoja kila siku kazi aliyoifanya kwa miaka 37, hatimaye akafanikiwa kukinusuru kisiwa cha MAJULI na ukame. JIFUNZE!! Kila hatua ndogo inauwezo wa kuleta mabadiliko makubwa katika maisha yako.
AMKA KIJANA pambana kama timu inayohitaji ushindi wa mechi moja ili kutwaa kombe, kwani mafanikio ya Kesho yanaanza na leo.