Mapacha wengi waliozaliwa kwa kuungana wametokea kupoteza maisha mda mfupi baada ya kuzaliwa kutoka na sababu mbalimbali kama upasuaji mfano ni LADAN na LALEH BIJANI mapacha wa kike waliozaliwa nchini Iran 1974, ambao walifariki mda mfupi baada ya kufanyiwa Upasuaji.
Hata hivyo hii ni rekodi ya baadhi ya Mapacha waliozaliwa wakiwa wameungana na wameishi mda mrefu zaidi bila upasuaji.
MGIACOMO na GIOVANNI BATTISTA TOCCI, ndio mapacha wa kwanza walioungana na kuweka rekodi ya kuishi umri mrefu. Mapacha hawa wenye jinsia ya kiume walizaliwa huko Locana, Italia mnamo mwaka 1877 na kudumu katika ulimwengu huu kwa miaka 63.
Akiwa na miaka 19 MARIA LUIGIA MEZZANROSA alijifungua watoto hao katika njia ya kawaida ya uzazi katika hospitali moja huko Italia, lakini baba wa watoto hao GIOVANNI TOCCI, alipata mshituko mkubwa baada ya kuona hali ya watoto wake lakini alirejea katika hali ya kawaida baada ya mwezi mmoja.
Mapacha hao walizungumza Kiitaliano, Kigerman na Kifaransa , mbali na mapacha hao kuungana, kitabia walikuwa na utofauti mkubwa, kwani GIACOMO alikuwa ni muongeaji sana tofauti na GIOVANNI aliyekuwa mtulivu.
Katika maisha yao mapacha hao walitembelea nchi nyingi za barani Ulaya kama Italia, Ujerumani, Ufaransa, na Uholanzi na pia mwaka 1892 waliwasili New York nchini Marekani katika ziara iliyowapa pesa nyingi na umaarufu mkubwa duniani. Hata hivyo maisha yao waliyamalizia huko VENICE, mji uliopo kaskazinimashariki mwa Italia.
Mbali na mapacha hao, CHANG na ENG BUNKER mapacha wa kiume waliozaliwa SAMUTSONGKRAM, karibu na Bangkok nchini Thailand mwaka 1811 na kufariki mwaka 1874 ni wengine walioungana na kuishi maisha marefu katika rekodi za dunia.
Kifo cha Mapacha hawa kilikuwa cha kitofauti kidogo kutokana na wao kutokushirikiana kwenye mfumo mzima wa upumuaji, kwani CHANG alipata mshituko kutoka na kunywa sana japo tatizo hilo halikumdhuru ENG, hata hivyo mwezi wa januari 1874, CHANG alifariki wakati ENG akiwa katika usingizi mzito na aliposhituka alilia sana baada ya kutambua kaka yake amefariki. Hata hivyo madaktari walijitahidi kufanya upasuaji wa kumtenganisha lakini hawakufanikiwa kwani masaa matatu baadaye naye aliungana na kaka yake katika safari ya mwisho hapa duniani.
Hata hivyo kulingana na GUINNESS WORLD RECORDS (2009) rekodi yao ya kuishi umri mrefu ilivujwa na RONNIE NA DONNIE GALYON, Mapacha wa kuungana waliozaliwa tarehe 28, 1951, katika hospital ya St. Elizabeth huko DAYTON, OHIO nchini Marekani wakiwa na umri wa miaka 64.
Maisha ya Mapacha hawa yanawashangaza wengi kwani, mbali na kuungana huko Mapacha hawa wanatazamana mda wote na kufanya mambo yao kwa wakati mmoja lakini hawajuani kabsa staili za maisha yao.
Mapacha hawa ni maarufu sana Duniani na wamefanya ziara nyingi katika majimbo ya nchini Marekani , Ulaya na Amerika ya kusini , mbali za ziara hizo Mapacha hawa wametokea kwenye shoo mbalimbali za Television kama The Jerry Springer show mwaka 1997, Discovery Channel Documentary 1998 na Channel Five Documentary ya mwaka 2009.
Kutokana na malipo waliyoyapata kutokana na ziara Mbalimbali na Maonyesho waliweza kujenga Nyumba yao binafsi mwaka 1991 huko DAYTON, OHIO nchini Marekani na kuanzisha Makazi katika nyumba hiyo, hata hivyo katika shughuli mbalimbali za kila siku wanasaidiwa na Kaka yao JIM na Mke wake MARY.
Hatahivyo Kuna Mapacha wengi zaidi ambao sijawaandika katika Makala hii japokuwa hawa ndio mapacha wenye rekodi kubwa Zaidi.
Unaweza Kudownload Na Kusikiliza Makala Hii Kwa Njia Ya Sauti.