Unaambiwa, Mwanamuziki wa Marekani wa mtindo wa rap B.o.B. anasaka msaada wa kutuma satelaiti kuthibitisha iwapo kweli dunia ni duara.
Jina lake halisi ni Bobby Ray Simmons Jr, Maarufu kama Rapa B.o.B ni mmojawapo ya watu wanaoamini kwamba Dunia ni kama sahani na sio duara.
Rapa B.o.B. Anajaribu kuchangisha $200,000 katika mtandao wa kuchangisha fedha wa GoFundMe na mpaka sasa amefanikiwa kukusanya kima cha $650, lakini kampeni hiyo imekuwa ikizungumziwa kwa mapana katika mtandao huo.
Katika video moja iliowekwa kwenye mtandao Rapa B.o.B. alisema Kuwa, Ameanzisha kampeni hiyo kwasababu angependa kutuma kama sio satelaiti moja basi nyingi katika anga za juu kujaribu kutafuta upinde unaoifanya dunia kuwa duara,".
Aliongeza Kuwa "Nautafuta upinde,".