HIZI NDIZO SABABU ZA CHUI KULA WINDO LAKE JUU YA MTI









Unaambiwa ni kitu ambacho kinaeleweka kuwa sicho cha kawaida kufanyika lakini Chui ana sababu nzuri za kuweza kufanya hivyo.

Baada ya windo lake kukamilika mara nyingi Chui husherekea chakula  chake juu ya mti kabla ya kuacha mifupa, ngozi na nyama nyama.
Mara nyingi Chui hupandisha kitoweo chake mtini kwani asipofanya hivyo huwa katika hatari ya kupoteza kwa fisi na simba.

Sasa, Utafiti uliofanywa na shirika moja lisilokuwa la serikali uligundua kuwa chui katika mbuga ya Sabi Sands huwawinda karibu familia 40 ya wanyama na Chui hupandisha mtini nusu ya wanyama anaowawinda.

Pia utafiti huo ulionyesha kuwa Chui hupoteza moja ya mawindo yake kati ya matano kwa wanyama wengine kama Fisi, Simba na hata Chui wa kiume.

Ikiwa chui ataamua kupandisha mtini windo lake na kisha kugundua kuna mshindani karibu anaweza kutafuta mti unaofaa ulio karibu na Mara chui anapokaribia mti hupanda hadi umbali wa mita10 juu kutafuta eneo lililo salama kwa kuning'iniza windo lake.

Hata hivyo wakati mwingine hali huwa ni ya dharura kama Fisi yuko karibu, Chui mara moja anaweza kupanda mti wowote ulio karibu kuzuia chakula chake kuibiwa.