Raia huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 65 alikuwa ameketi kando ya dereva wakati akisafiri kuelekea karibu na mji wa Schwaz magharibi mwa Austria siku ya Jumamosi.
Alitoka katika kiti chake wakati gari hilo lilipogonga kizuizi cha mti kilicho kando ya barabara na kukanyaga breki Wakati basi likielekea chini ya mlima.
Gari hilo lililokuwa likipitia eneo la milima likiwa na abiria 21 lilinusurika kupata ajali kutokana na dereva mwenye umri wa miaka 76 kuzimia. Watu wanne walipelekwa hospitalini.