BWANAHARUSI AJITOSA MTONI NA KUMUOKOA MTOTO ANAYEZAMA


Unaambiwa,  Shughuli ya kupiga picha kwa Bwana na Bibi harusi iligeuka ghafla wakati bwana harusi aliporuka na kuingia mtoni kumuokoa mvulana mdogo aliyekuwa anazama.

Clayton na Brittany Cook walikuwa wanapiga pozi kwa picha zao walizokuwa wanapigwa baada ya harusi katika daraja la bustani huko Cambridge, Ontario, wakati bwanaharusi alipomuona mtoto huyo akitaa taa ndani ya mto.

Pasi kufikiria hata suti aliyovaa, Bwana Cook aliruka mtoni na kumvuta mtoto huyo hadi ufukweni. Cook anasema Kwa Muda wa dakika kadhaa watoto walikuwa wamesimama karibu na mto na baada ya muda akaona mtoto ndani ya maji akitapatapa huku akiinua kichwa chake juu ya maji na ndipo aliporuka ndani ya maji na kumvuta nje ya  maji.

Hata Hivyo Mkewe Clayton anasema awali alifikiria kuwa aliruka mtoni ki mzaha lakini punde tu alipogeuka alimkuta tayari alikuwa  amekwisha mvuta nje ya mto na aliendelea kupiga picha tukio zima.

Baada ya kuokolewa mtoto huyo alionekana ana uoga kiasi lakini alikaa sawa na baada ya mda akaaondoka na Kaka yake mkubwa. Hata Hivyo Mkewe amesema kuwa uwezo wa kufikiria kwa haraka wa mme wake ni baadhi ya mambo yaliyomfanya akubali kuolewa.