Unaambiwa, kwa mujibu wa ripoti ya tafiti iliyofanywa na jarida la Nature Neuroscience inaonesha kuwa watu waliowahi kuwasaliti wenza wao kwenye mahusiano kamwe hawataacha tabia hiyo mpaka mwisho wa mahusiano yao.
Utafiti huo unaonesha kuwa Mwanaume au Mwanamke akishachepuka ubongo hujenga tabia ya kudanganya na kuanza kuongeza tamaa ya kutokuridhika hivyo hata kama akiwa kwenye Ndoa au Mahusiano ya kawaida ni ngumu kubaki na mtu mmoja.
Hata hivyo utafiti huo umeonesha Msaliti hata kama akikamatwa na mwenza wake mara kadhaa hujutia tu kwa muda lakini baadae hurudia tabia hiyo kutokana na mwenendo wa ubongo na mara nyingi muhusika hutumia akili nyingi kumdanganya mwenzie.
Utafiti huo uliohusisha wanandoa 2,800 waliowahi kuchepuka kwenye ndoa zao kutoka barani Ulaya, Amerika Kaskazini na Afrika na umeonesha asilimia 89% ya wanandoa waliowahi kuchepuka kwenye ndoa zao wamekiri bado wanaendelea na mchezo huo kwa siri huku asilimia 10% wakisema wanatamani ila wanawaheshimu wenzawao huku asilimia 1% ndiyo wamesema wameacha mchezo huo.